Mwalimu Maganga Japhet asimamishwa kazi kwa utoro

DAR ES SALAAM-Mwalimu Maganga Japhet amesimamishwa kazi na Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) kutokana na tuhuma za utoro kazini na kukaidi au kukataa kutekeleza maelekezo halali ya viongozi wake.
Taarifa za kusimamishwa kwa Maganga ambaye ni Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), zimetolewa kupitia barua ya taarifa kwa umma iliyosainiwa na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Manispaa ya Temeke, Fransisca Mselemo.

Barua hiyo imeeleza kuwa, Maganga amesimamishwa kazi na Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, Elihuruma Mabelya chini ya Tume ya Utumishi wa Walimu ambayo ndiyo yenye mamlaka ya nidhamu ya walimu.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa uamuzi wa kusimamishwa kazi Maganga, ulifikiwa Desemba 5, 2023 ambapo kabla ya kusimamishwa, Maganga alikuwa Mwalimu wa Shule ya Msingi Tandika iliyopo jijini Dar es Salaam.

Awali, Maganga aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera na Rais Samia Suluhu Hassan ingawa ilielezwa kwamba hakuitikia uteuzi huo na kuendelea kusalia kuwa Katibu Mkuu wa CWT.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news