MOROGORO-Mkazi wa Kijiji cha Kikweta kilichopo Kata ya Lumemo, Halmashauri ya Mji Ifakara katika Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro, Petronila Ngurukila ametoa msaada wa pikipiki moja aina ya Houjue kwa Polisi Kata ya Lumemo.
Afisa huyo wa polisi amekuwa akitumia usafiri wa baiskeli kwa ajili ya kutoa elimu ya ulinzi shirikishi kwa wananchi wa vijijini ili kurahisishia utendaji wake wa kazi.
Ngurukila ambaye ni mfanyabiashara katika kijiji hicho amekabidhi pikipiki hiyo kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Alex Mkama kwenye halfa iliyofanyika katika Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Kilombero kilichopo mjini Ifakara.
Amesema,amefikia uamuzi wa kutoa msaada wa pipikipi mpya kutokana na mazingira aliyokuwa akiyapitia Afisa huyo ya kutumia baiskeli kuwafikia walengwa, na kuunga mkono juhudi na jitihada za Jeshi la Polisi kuzuia uhalifu.
Polisi Kata wa Kata ya Lumemo, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Edwin Kipimo amesema,kwa mura mrefu alikuwa anatumia usafiri wa baiskeli kwa ajili ya kwenda kutoa elimu kwa wananchi wa vijiji vilivyopo kwenye kata hiyo.
Amesema,katika majukumu yake hukabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ugumu wa kuwafikia wananchi kwa wakati kutokana hali ya kijiografia na ukubwa wa kata hiyo.