Naibu Waziri Pinda asisitiza matumizi bora ya ardhi

NA MUNIR SHEMWETA
WANMM MLELE

NAIBU Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda amewaasa watanzania kuhakikisha wanakuwa na mipango bora ya matumizi ya ardhi kwa manufaa ya sasa na vizazi vijavyo kwa kuwa ardhi iliyopo haiongezeki na idadi ya watu inazidi kuongezeka.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda akizungumza na mmoja wa wananchi waliohudhuria hafla maalum ya chakula aliyowaandalia wananchi na viongozi wa jimbo lake kusheherekea Sikukuu ya Chrismas tarehe 26 Desemba 2023 nyumbani kwake Kibaoni mkoani Katavi. Wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mpimbwe, Shamimu Mwariko. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI).

Mhe. Pinda amesema hayo Desemba 26, 2023 nyumbani kwake Kibaoni, Halmashauri ya Mpimbwe mkoani Katavi katika hafla maalum ya chakula aliyowaandalia wananchi na viongozi wa jimbo lake kusheherekea Siku Kuu ya Chrismas.

Katika hafla hiyo iliyohudhuriwa pia na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa na Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda, Naibu Waziri huyo wa Ardhi alisema, wakati serikali ikiandaa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050, watanzania wanatakiwa kuwa na mpango wa matumizi ya ardhi huku wakielewa changamoto kubwa iliyo mbele yao ni kuwa ardhi haiongezeki.
Sehemu ya wananchi wa jimbo la Kavuu katika halmashauri ya Mpimbwe wakiwa kwenye hafla maalum ya chakula kilichoandaliwa na Mbunge wa jimbo hilo ambaye ni Naibu Waziri wa Ardhi Mhe. Geophrey Pinda kusheherekea Siku Kuu ya Chrismas tarehe 26 Desemba 2023. Hafla hiyo imefanyika nyumbani kwake Kibaoni mkoani Katavi.

‘’Miaka 25 inayokuja lazima tufikirie hizi hekta na ekari tulizopopewa na Mungu ikaitwa Tanzania inatushoje itakapofika miaka hamsini ijayo, kwa hiyo ni sisi ndiyo tutakaopanga tutumiaje maeneo yetu,’’ alisema Mhe. Pinda.

‘’Kila mtu akikaa ajue ardhi ni yake na ndugu zake kwa hiyo tuishi kwa amani na tusigombane, hakuna namna tutakachokifanya katika eneo hili ni lazima tukubaliane namna ya kuitumia ardhi ndogo katika ongezeko kubwa la watu,’’alisema Pinda.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda akizungumza wakati hafla maalum ya chakula alichowaandalia wananchi na viongozi wa jimbo lake kusheherekea Siku Kuu ya Chrismas tarehe 26 Desemba 2023 nyumbani kwake Kibaoni mkoani Katavi.

Akigeukia shughuli za maendeleo kwenye jimbo lake la Kavuu, Mhe Pinda amewaambia wananchi wake kuwa, jimbo hilo kwa sasa limepiga hatua kubwa ukilinganisha na miaka ya nyumba kwa kuwa Rais Samia Suluhu Hassan amewezesha utekelezaji miradi mbalimbali ya maendeleo hata ile ambayo haikutajwa kwenye ilani ya CCM na kutolea mfano ujenzi wa zahanati, shule na miundombinu.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mpimbwe mkoa wa Katavi Shamimu Mwariko akizungumza katika hafla malum ya chakula iliyoandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Kavuu ambaye ni Naibu Waziri wa Ardhi Mhe. Geophrey Pinda kwa wananchi na viongozi wa jimbo lake kusheherekea Siku Kuu ya Chrismas tarehe 26 Desemba 2023 nyumbani kwake Kibaoni mkoani Katavi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mpimbwe, Shamimu Mwariko aliwapa ushauri wananchi wa Mpimbwe kuwa, kama wanataka halmashauri yao ifanane kimaendeleo na halmashauri zilizopiga hatua kubwa kimaendeleo basi wahakikishe wanawashika viongozi wanaofanya maamuzi ya kimkakati.

‘’Kama kweli mna lengo la kusema sasa sisi Mpimbwe iwe inafanana na eneo fulani shikeni viongozi wanaofanya mamuzi kimkakati, utekelezaji wao, mipango yao ni kuhakikisha wanafungua njia watu waweze kupita njia hizo ndiyo kazi ya kiongozi yoyote duniani,"alisema Shamim.
Sehemu ya wananchi wa jimbo la Kavuu katika halmashauri ya Mpimbwe wakiwa kwenye hafla maalum ya chakula kilichoandaliwa na Mbunge wa jimbo hilo ambaye ni Naibu Waziri wa Ardhi Mhe. Geophrey Pinda kusheherekea Siku Kuu ya Chrismas tarehe 26 Desemba 2023. Hafla hiyo imefanyika nyumbani kwake Kibaoni mkoani Katavi.

Naye Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa na Waziri Mkuu mstaafu Mhe. Mizengo Pinda amemtaka Mbunge wa Jimbo la Kavuu ambaye ni mdogo wake kuwa karibu na wananchi wakati wote wa juhudi mbalimbali za kuliletea maendeleo jimbo lake.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa ambaye ni Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda akizungumza katika hafla maalum ya chakula kilichoandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Kavuu ambaye ni Naibu Waziri wa Ardhi Mhe. Geophrey Pinda kwa wananchi wa jimbo lake kusheherekea Siku Kuu ya Chrismas tarehe 26 Desemba 2023.

‘’Hoja kubwa ya wananchi unaowaoongoza ni mahusiano, mnaishije? Kila aliyesimama amekupa sifa ni jambo zuri kazi yako sasa ni kutoharibu sifa, kaza uzi na jishushe kadri inavyowezekana na watu wote ni wa kwako hata wale mliopingana,’’ alisema Mizengo Pinda.
Sehemu ya wananchi wa jimbo la Kavuu wakiwa kwenye hafla maalum ya chakula ilyoandaliwa na Mbunge wa jimbo hilo ambaye ni Naibu Waziri wa Ardhi Geophrey Pinda kusheherekea Siku Kuu ya Chrismas tarehe 26 Desemba 2023.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Mhe. Geophrey Pinda yuko jimboni kwake katika Halmashauri ya Mbimbwe mkoa wa Katavi kujumuika wananchi wa jimbo la Kavuu pamoja na mambo mengine kusheherekea Siku Kuu ya Chrismas na wananchi wa jimbo lake.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news