Ofisi ya Msajili wa Hazina yang’ara Tuzo za NBAA

DAR ES SALAAM-Ofisi ya Msajili wa Hazina imeng’ara kwa kuibuka mshindi wa kwanza katika tuzo za uandaaji wa taarifa za fedha kwa mwaka 2023 katika kundi la Idara Huru za Serikali (Independent Government Department).
Mkurugenzi wa usimamizi wa Utendaji, Ufuatiliaji na Tathmini – Mashirika ya Kibiashara, Bi. Lightness Mauki (kulia), akipokea tuzo kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, CPA Jamal Kassim Ally (kushoto) wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo zilizondaliwa na Bodi ya Taifa ya uhasibu na ukaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), katika hafla iliyofanyika mwishoni mwa wiki Jijini Dar es Salaam. (wa pili kulia). ni Mkurugenzi wa Fedha na Uhasibu wa Taasisi hiyo Hassan Mohamed.

Tuzo hizo zimetolewa mwishoni mwa wiki na Bodi ya Taifa ya uhasibu na ukaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Ofisi ya Msajili wa Hazina iliwakilishwa na Mkurugenzi wa Usimamizi, wa Utendaji, Ufuatiliaji na Tathmini – Mashirika ya Kibiashara, Bi. Lightness Mauki akiambatana na Mkurugenzi wa Fedha na Uhasibu wa Taasisi hiyo Hassan Mohamed, kwa niaba ya Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu.

Akizungumza mara baada ya kupokea tuzo hiyo, Bi. Mauki amesema kuwa ushindi walioupata utaongeza chachu ya kufanya kazi kwa ufanisi zaidi na kuimarisha utendaji kazi katika taasisi yao.

Bodi ya Taifa ya uhasibu na ukaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) imekuwa na utaratibu wa kila mwaka kutoa tuzo kwa Mashirika na Taasisi za Serikali zilizofanya vizuri kutambua kazi wanazofanya.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news