Operesheni maalum yakamata watuhumiwa 70 maeneo ya kitalii Zanzibar

ZANZIBAR-Katika kukabilianana na kero wanazofanyiwa watalii katika fukwe mbalimbali, Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Kaskazini Unguja imefanya operesheni maalum na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa 70 kwa makosa mbalimbali.
Akizungumza na waandishi wa habari huko ofisini kwake Mkototoni, Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Ungujaambaaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa mkoa huo, Mheshimiwa Rashid Hadid Rashid amesema, operesheni hiyo ni maagizo ya Mhe. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dkt.Hussein Ali Mwinyi ya kuwataka wakuu wa Mikoa kuweka mazingira salama kwa wananchi na watalii katika maeneo yao.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja, Kamishna Msaidizi wa Polisi Daniel Shila ameeleza kuwa, miongoni mwa waliokamatwa katika Operesheni hiyo ni Twalib Shaaban Zuberi (39) raia wa Kenya ambaye amekamatwa na dawa za kulevya.

Aidha,amesema Jeshi la Polisi litaendelea kushirikiana na Vikosi vya Ulinzi na Usalama katika operesheni hizo ili kuhakikisha Mkoa huo unaendelea kuwa salama kwa wananchi na kuendelea kuvutia watalii.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news