NA FRESHA KINASA
KATIKA kuandaa wasomi wenye ujuzi na maarifa kwa jamii na taifa, Shule ya Sekondari Etaro iliyopo katika Jimbo la Musoma Vijijini Mkoani Mara imedhamiria kuwa na "High School'' ya Somo la Kompyuta kuanzia mwakani.
Hayo yamebainishwa na taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini chini ya Prof.Sospeter Muhongo Desemba 20, 2023.
Taarifa hiyo imesema kuwa, harambee itafanyika tarehe 23, 12, 2023 kuanzia majira ya saa tatu asubuhi Shuleni Etaro Kijijini hapo. Wadau mbalimbali na wazawa wa Jimbo la Musoma Vijijini wameombwa kushiriki harambee hiyo kuwezesha uchangiaji kupitia
"Akaunti ya Shule
Benki: NMB Musoma
Akaunti Na: 30301200341Jina la Akaunti: Etaro Sekondari"
Maabara zilizoko Etaro Sekondari
(i) Maabara ya Bailojia
Ilishajengwa na tayari inatumiwa
(ii) Maabara ya Kemia
Serikali imetoa Tsh milioni 30 (Tsh 30m) kwa ujenzi wa maabara hii ambayo itakamilika kabla ya tarehe 15.1.2024. Tunaishukuru sana Serikali yetu kwa mchango huu.
(iii) Maabara ya Kompyuta
Kompyuta 25 zimefungwa kwa msaada ya fedha kutoka Chuo Kikuu cha Northern Illnois, USA. Tunakishukuru sana Chuo hiki kwa mchango huu.
Mafunzo ya Kompyuta yameanza kutolewa wiki hii hapo shuleni kwa kutumia Wahadhiri wa DIT ambao ndio wamepewe jukumu la kujenga Maabara ya Kompyuta shuleni hapo.
Headmaster Jacob Joseph Chagavalye na walimu wenzake, wanapongezwa sana kwa ubunifu wao na udumishaji mzuri wa urafiki wao na Northern Illnois University - mfadhili wa Computer Lab ya Etaro Sekondari.
(iv) Maabara ya Fizikia
Harambee ya Mbunge wa Jimbo itachangia ujenzi wa maabara hii ambayo imepangwa ikamilike kabla ya tarehe 1.3. 2024
"High School" ya Somo la Kompyuta:
Etaro Sekondari inajitayarisha (mwakani, Julai 2024) kuwa na Form V yenye mchepuo wa Physics, Mathematics & Computer Science na michepuo mingine ya masomo ya sayansi."
"Taarifa nyingine za Etaro Sekondari,
Sekondari ya Etaro ilifunguliwa Mwaka 2006. Sekondari hii inahudumia vijiji vinne vya Kata ya Etaro. Vijiji hivyo ni: Busamba, Etaro, Mmahare na Rukuba (Kisiwa)"
"Etaro Sekondari ina wanafunzi 897. Wanafunzi wa Kidato cha nne (Form IV) wanaosoma somo la Fizikia ni 20 kati ya 146 (13.7%), na wale wanaosoma somo la Kemia ni 41 kati ya 146 (28.1%)"
HARAMBEE NA MCHANGO WAKO
"Unakaribishwa sana kwenye Harambee yetu ya Jumamosi, 23.12.2023.Iwapo utashindwa kuhudhuria Harambee hiyo, tafadhali sana MCHANGO wako utume moja kwa moja kwenye Akaunti ya Etaro Sekondari,"
"Tuweke miundombinu ya elimu ya Sayansi Kwenye shule zetututawashawishi na kuwavutia wanafunzi wengi kuwa wanasayansi," imeeleza taarifa hiyo.