ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameipongeza Serikali ya Saudi Arabia kwa jitihada kubwa wanayoitoa Tanzania kuunga mkono miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo Sekta ya Afya, Maji, Miundombinu ya Barabara na kusaidia uzalishaji umeme.
Rais Dkt. Mwinyi amesema hayo alipozungumza na Balozi wa Saudia Arabia nchini Tanzania, Mhe. Yahya Ahmed Okeish na ujumbe wake Ikulu Zanzibar tarehe 8 Desemba 2023.
Aidha Rais Dkt. Mwinyi aliikaribisha Serikali ya Saudia Arabia kuwekeza kwenye shamba la Makurunge, Bagamoyo linalomilikiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, ambalo linafaa kwa uwekezaji wa kilimo, Uvuvi na Utalii.
Kwa upande mwingine Rais Dkt. Mwinyi aliipongeza Timu ya Madaktari 21 kutoka Saudia Arabia waliojitolea kuweka kambi ya matibabu na upasuaji jimbo la Gando, Mkoa wa Kaskazini Pemba.