Rais Dkt.Mwinyi aishukuru Qatar kwa kufadhili mradi wa kurudisha watoto shuleni Zanzibar

DOHA-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi amekutana na mtoto wa Amiri wa zamani wa Qatar ambaye pia ni Mwenyekiti wa Makumbusho ya Taifa,Mhe. Sheikha Al Mayassa bint Hamad bin Khalifa Al Thani katika Hoteli ya Sheraton ambapo ndipo linapofanyika Jukwaa la Doha (Doha Forum) tarehe 10 Desemba, 2023.
Rais Dkt. Mwinyi amemshukuru Mhe. Sheikha Al Mayassa kwa niaba ya Serikali ya Qatar kupitia mradi wa miaka mitatu wa Out Of School Children (OOSC) uliofadhiliwa na Qatar Fund for Development ambao umetekelezwa kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la UNICEF pamoja na Education Above All Foundation (EAA).

Aidha, Rais Dkt. Mwinyi amesema,mradi huo umefanikiwa kwa kiasi kikubwa baada ya kuwarudisha shuleni watoto zaidi ya 35,500 Unguja na Pemba na kuendelea na masomo.

Rais Dkt. Mwinyi pia amependekeza kwa Mhe. Sheikha mpango wa kubadilishana wanafunzi katika fani ya Ukutubi kutoka Zanzibar kuja kujifunza na kubadilishana uzoefu na maarifa katika Maktaba ya Doha.

Kabla ya kumaliza mkutano huo, Rais Dkt. Mwinyi amemweleza Mhe. Sheikha kuwa Zanzibar ina utajiri wa Mambo ya Kale hivyo kutokana na uzoefu mzuri wa Qatar katika masuala hayo, ingekuwa ni fursa nzuri kusaini Mkataba wa Makubaliano (MOU) hii itawawezesha wataalamu kutoka Qatar kubadilishana uzoefu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news