ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi amejumuika pamoja na uongozi wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Ushirikiano wa Elimu Duniani (GPE) ukiongozwa na Mwenyekiti wake, Dkt.Jakaya Kikwete, Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ni katika chakula cha usiku ambacho Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi mewaandaliwa Desemba 4, 2023 Ikulu jijini Zanzibar.

Hafla hiyo pia imehudhuriwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa GPE, Laura Frigenti pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali, Dini na Vyombo vya ulinzi na usalama.
Aidha,vikao vya GPE vitafanyika Zanzibar na kufunguliwa Desemba 5 hadi 6, mwaka huu ikiwa ni mara ya kwanza kwa shirika hilo la kimataifa kufanya vikao vyake vya bodi barani Afrika.
Vilevile shirika hilo limeisaidia Zanzibar katika sekta ya elimu fedha za kigeni dola za kimarekani milioni 11.7 kwa ajili ya kusaidia elimu ya msingi ikiwemo miradi itakayoanza Januari 2024 kwa kujumuisha mafunzo ya walimu, utendaji, usimamizi wa elimu , masuala ya jinsia na mjumuisho.
Kwa mujibu wa Dkt. Kikwete, ambaye ni Mwafrika wa kwanza kuongoza GPE, shirika hilo hadi sasa limeishaipatia Tanzania jumla ya Dola za Kimarekani Milioni 332 (takriban shilingi 834,980,332,000.00) ili kusaidia sekta ya elimu bara na Zanzibar.