Rais Dkt.Mwinyi:Manyara poleni, Zanzibar ipo pamoja nanyi katika kipindi hiki kigumu

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi ameelezea kupokea kwa masikitiko makubwa na mshtuko taarifa za mafuriko na maporomoko ya udongo yaliyosababisha vifo vya watu zaidi ya 50.

Sambamba na majeruhi 85, uharibifu mkubwa wa mali na miundombinu katika Kijiji cha Katesh mkoani Manyara tarehe 3 Desemba, 2023.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Desemba 4, 2023 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Charles Hillary.

Aidha, Rais Dkt.Mwinyi ameunga na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan kutuma salamu za pole kwa wananchi wa Mkoa wa Manyara kufuatia maafa hayo.

"Zanzibar ipo pamoja nanyi katika kipindi hiki kigumu," amesema Rais Dkt.Mwinyi huku akiwaombea kwa Mwenyenzi Mungu waliopoteza maisha na wale walioathirika kwa kupoteza mali zao kutokana na mafuriko ili warejee katika hali zao za kawaida kwa haraka.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news