Rais Dkt.Samia ahutubia katika Mkutano wa COP28 UAE

ABU DHABI-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameyataka mataifa duniani kutambua kuwa suluhisho la uhakika la kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi ni kutimiza ahadi za kutoa fedha na kuongeza kasi ya mikakati ya kukabiliana na janga hilo.

Rais Samia ametoa tamko hilo leo katika mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP28) uliofanyika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).

Aidha, Rais Samia amesema ilitolewa ahadi ya dola za Kimarekani bilioni 100 kila mwaka, ili kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi katika mkutano wa Copenhagen na ahadi hiyo haijatekelezwa licha ya kiasi hicho kuwa kidogo kuliko kilichohitajika.

Kwa upande mwingine, Rais Samia amesema mkutano wa Paris na Ufaransa iliazimiwa kudhibiti ongezeko la joto chini ya nyuzi joto 1.5, lakini hali ni kinyume kwani kasi ya ongezeko la joto kwa sasa duniani inatia wasiwasi.

Rais Samia pia amesema kushindwa kutimiza ahadi kunapunguza mshikamano na imani na kuleta matokeo mabaya kwa nchi zinazoendelea, ikiwemo Tanzania,ambayo hupoteza kati ya 2% hadi 3% ya Pato la la Taifa (GDP) kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Akisisitiza kwenye mkutano huo, Rais Samia amesema Tanzania ina nia ya kuhamasisha kuongezwa matumizi ya nishati safi na gharama nafuu ya kupikia na teknolojia kote barani Afrika, hasa kwa wanawake.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news