Rais Dkt.Samia atunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Heshima ya Utalii na Usimamizi wa Masoko

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano Samia Tanzania,Mheshimiwa Dkt.Suluhu Hassan amewataka wanafunzi wa vyuo vikuu nchini kuleta mabadiliko chanya katika jamii mara wanapohitimu masomo yao.

Dkt.Samia ameyasema hayo Desemba 28,2023 jijini Zanzibar katika Mahafali ya 19 ya Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA).

Mheshimiwa Rais Dkt. Samia ameeleza kuwa, amefarijika kuona wanawake wanazidi kuhamasika katika elimu nchini.

“Nimepata faraja kuona asilimia 58 ya wahitimu leo ni wanawake,” amesema Rais Dkt.Samia.
Kupitia chuo hicho mbacho Mkuu wake ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Mwinyi, kimemtunuku Rais Dkt. Samia Shahada ya Uzamivu ya Heshima ya Utalii na Usimamizi wa Masoko kwa kutambua mchango wake wa kuifungua nchi kiuchumi kupitia Sekta ya Utalii.

“Kwa heshima na unyenyekevu mkubwa nimesimama mbele ya umma huu kukubali shahada hii,"amesema Rais Dkt.Samia.

Awali, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Lela Mohammed Mussa amesema kwa kazi kubwa ambayo Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa akiifanya tangu ashike hatamu ya urais nchini nastahili kupewa Uprofesa.

“Nataka niungane na wote ambao wametoa wasifu wa Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa anastahili kupewa tuzo na sio tu katika ngazi ya PhD, lakini kwa kazi kubwa ambayo amekuwa akiifanya tangu ashike hatamu anastahili Uprofesa.

“Uthubutu mkubwa ambao amekuwa akionesha katika uongozi wake, ukomavu wa kisiasa na uvumilivu wa hali ya juu ni zaidi ya PhD na niliuliza wakati linakuja wazo la Rais Samia kupewa PhD nikauliza, kwani haiwezekani kumpa Uprofesa moja kwa moja tukamaliza kazi, nikaambiwa kuna taratibu zake,lakini Mheshimiwa tutazishughulikia.

Aidha,kwa Rais Dkt. Samia hii ni PhD ya tatu ametunukiwa tangu awe Rais wa Tanzania, ya kwanza alikabidhiwa UDSM na Rais mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete na hii ya SUZA amekabidhiwa na Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

Pia, hivi karibuni Rai Dkt.Samia alitunukiwa udaktari wa heshima (PhD) na Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru (JNU) nchini India.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news