NA DIRAMAKINI
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan akiwemo Rais wa 31 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson wametajwa kuwa miongoni mwa Wanawake 100 wa Afrika wenye ushawishi zaidi kwa mwaka 2023, kulingana na orodha iliyotolewa na Avance Media.
Chapisho hilo la 2023 lililochaguliwa kwa ajili ya michango yao ya kipekee kwa sekta mbalimbali barani, lina marais, makamu wa rais, viongozi 20 kutoka sekta ya biashara, wanadiplomasia 24, viongozi sita vinara katika mabadiliko ya tabia nchi.
Pia,, viongozi 21 kutoka AZAKI na uhisani na kategoria zingine mashuhuri kama vile utawala, vyombo vya habari, michezo na burudani.
Mkusanyiko huo unalenga kuwaangazia wanawake wanaoongoza mipango yenye matokeo chanya barani Afrika, wakitumika kama vielelezo vya kusisimua kwa kizazi kijacho.
Kwa mujibu wa Avance Media, vigezo vya uteuzi vilijumuisha ubora katika uongozi na utendaji, mafanikio binafsi, kujitolea kubadilishana maarifa, kuvunja hali iliyopo na kuwa mwanamke Mwafrika aliyekamilika na shupavu;