Rais Dkt.Samia:Kinu cha kwanza JNHPP kitawashwa Januari,2024

DAR ES SALAAM-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan amesema, katika kuondoa changamoto za umeme zilizopo kwa sasa nchini, Serikali itawasha kinu cha kwanza cha kufua umeme katika Bwawa la Mwalimu Nyerere (Julius Nyerere Hydroelectric Power Plant (JNHPP) ifikapo Januari 2024.

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi, wafanyabiashara pamoja na wageni mbalimbali wakati wa hafla ya utoaji tuzo za Rais kwa Wazalishaji Bora nchini (PMAYA) iliyofanyika katika ukumbi wa Super Dome , Masaki Jijini Dar es Salaam tarehe 17 Desemba, 2023.

Mheshimiwa Rais Dkt.Samia ametoa kauli hiyo Desemba 17, 2023 wakati akizungumza katika utoaji wa tuzo za Rais kwa Wazalishaji Bora nchini (President’s Manufacturer of the year Awards-PMAYA) kwenye ukumbi wa Super Dome, Masaki jijini Dar es Salaam.

"Jumla ya vinu vyote viko tisa cha kwanza kitawashwa Januari, cha pili hakitozidi Aprili, vile vinu viwili tukiwasha tutakuwa na umeme wa kutosha sana,"amebainisha Mheshimiwa Rais Dkt.Samia.

Akizungumzia kuhusu suala la upatikanaji wa dola, Mheshimiwa Rais Dkt.Samia amesema kuwa, “Tanzania we're far better angalau sisi tunamudu kuongeza kiasi cha kutoa kwa siku, ilipokuwa crisis kali tulikuwa tunatoa dola laki tano kwa mtu kwa siku, tukapandisha milioni moja,tukapandisha hadi milioni mbili."

Pia, Mheshimiwa Dkt.Samia amewataka wazalishaji wa bidhaa kupitia Shirikisho la Wenye Viwanda Nchini (CTI) kuendelea kuimarisha ubora wa bidhaa wanazozalisha nchini.

Aidha, Rais Samia amesema serikali imeimarisha miundombinu ya barabara na
bandari ili bidhaa zinazozalishwa zisafirishwe nje na kuingia nchini ili sekta ya
viwanda iendelee kufanya vizuri.

Rais Samia pia amewataka wazalishaji hao kuongeza juhudi katika uzalishaji na uongezaji wa bidhaa (intermediate goods) ili kupunguza utegemezi wa bidhaa kutoka nje ya nchi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news