RUVUMA-Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi,SACP Ramadhani Ng’anzi amewataka abiria wanaosafiri ndani na nje ya Mkoa Ruvuma kutoa taarifa za baadhi ya madereva wanaokiuka sheria za usalama barabarini.
SACP Ng’anzi ameyasema hayo alipotembelea Kituo Kikuu cha Mabasi kilichopo eneo la Shule ya Tanga ndani ya Manispaa ya Songea Mkoa wa Ruvuma.
Amesema kuwa, huo ni mwendelezo wa ziara yake ya ukaguzi wa vyombo vya moto mkoani humo.
Pia,SACP Ng’anzi amewaonya madereva wenye tabia ya ulevi pamoja na kuendesha magari kwa mwendo kasi na watakaobainika watachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo ya kunyang’anywa leseni zao.