NA DIRAMAKINI
WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Moses Nnauye (MB) amethibitisha kuwa, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepata nafasi katika Orbit kwa ajili ya Setelaiti.
Mheshimiwa Waziri Nape ameyabainisha hayo kupitia ukurasa wake wa X huku akifafanua kuwa, hayo ni matokeo ya Mkutano wa WRC23.
"Tumefanikiwa kupata nafasi katika Orbit kwa ajili ya matumizi ya setelaiti. Orbit mpya ya setelaiti kwa Tanzania ni nyuzi (16 W).
"Mafaniko haya ni moja ya matokeo ya mkutano wa Umoja wa Mawasiliano Duniani-2023(WRC23)! Ahsante Rais Samia kwa Uongozi uliotukuka!."