Sera ya Elimu na Mafunzo (2014) na Mitaala Iliyoboreshwa (2023):Musoma Vijijini tuendelee kujitayarisha

MARA-Jimbo la Musoma Vijijini tuendelee kujenga na kuboresha miundombinu ya elimu itakayo kuwa rafiki kwa utekelezaji wa sera ya elimu na mitaala yake, itakayoanza kutekelezwa kwa awamu kuanzia mwakani.

(1) Kata ya Nyamrandirira

Kata hii ina vijiji vitano (5) vyenye sekondari mbili (2)

Kijiji cha Kaboni hakina shule yake ya msingi, kinatumia shule za msingi tatu (3) za Kijiji cha Kasoma.
Ujenzi wa Shule Shikizi Kaboni

Diwani wa Kata ya Nyamrandirira na Viongozi wa Kijiji cha Kaboni watafanya matayarisho ya kuanza kujenga Shule Shikizi Kaboni.

Mbunge wa jimbo atapiga harambee ya kuanza ujenzi huo.

Shule Shikizi Karusenyi

Shule hii inajengwa Kijijini Mikuyu, Kata ya Nyamrandirira. Ujenzi wa kuipanua umesimama.

Mheshimiwa Diwani wa Kata na Viongozi wa Kijiji cha Mikuyu wataweka mipango ya kufufua na kuendeleza ujenzi wa Shule Shikizi hii iwe shule ya msingi kamili, inayojitegemea.

Mbunge wa Jimbo alichangia mabati 50 kwenye ujenzi wa awali, ataendelea kuchangia ujenzi wa shule hii.

(2) Kata ya Nyakatende

Kata hii ina vijiji vinne (4) vyenye sekondari mbili (2)

Shule Shikizi Kiunda

Shule hii inajengwa kwenye Kitongoji cha Kiunda, Kijijini Kamguruki, Kata ya Nyakatende.

Wanafunzi wa shule hii watatoka kwenye vitongoji vitatu vya Bhusuna, Nyarubamba na Kiunda

Ujenzi uliokwishafanyika:

(i) Boma moja kubwa lenye vyumba vya madarasa mawili (2) na ofisi moja (1) ya walimu

(ii) Choo chenye matundu sita (6) kinaendelea kujengwa.

(iii) Ujenzi ulianza Mwaka 2020, na Mbunge wa Jimbo alianza kuchangia ujenzi huo kwa kutoa Saruji Mifuko hamsinihamsini.
Diwani wa Nyakatende na Kamati ya ujenzi ya Shule Shikizi Kiunda wanafufua na kuendeleza ujenzi huu.

Mbunge wa Jimbo ataitwa kupiga Harambee ya ujenzi huo.

Shule Shikizi zilizokwishasajiliwa

(3) Kata ya Makojo

Shule ya Msingi Mwikoko ilianza kujengwa Mwaka 2016 ikiwa Shule Shikizi

Michango ya awali ya ujenzi ilitolewa na Wana-kitongoji (Mwikoko) na Mbunge wao wa Jimbo, na baadae Serikali Kuu ilitoa michango mikubwa ya fedha.

Shule hii yenye madarasa mawili ya awali, na mengine manne (Std I-IV), ina vyumba vitano (5) vya madarasa, vingine viwili vinakamilishwa. Ofisi za walimu zipo mbili (2), nyingine moja inakamilishwa ujenzi. Matundu ya vyoo ni: 11 ya wanafunzi na 2 ya walimu.

(4) Kata Tegeruka

Shule ya Msingi Nyasaenge (awali ikiwa shule shikizi) ilianza kujengwa Mwaka 2018 kwa michango ya Wana-Kitongoji (Nyasaenge) na Mbunge wao wa Jimbo.

Baadae Serikali Kuu ilitoa michango mikubwa ya fedha na kuwezesha shule hii kupata vyumba saba (7) vya madarasa, ofisi mbili za walimu, vyoo vyenye matundu 16 ya wanafunzi na 2 ya walimu.

Shule hii ina madarasa mawili ya awali, na mengine saba (Std I-VII).

(5) Kata ya Etaro

Shule ya Msingi Egenge iko Kijijini Busamba ndani ya Kitongoji cha Egenge. Shule ina madarasa ya awali mawili na mengine manne (Std I- IV)

Shule ilianza ikiwa shule shikizi iliyoanza kujengwa kwa nguvu za Wana-Kitongoji (Egenge) na Mbunge wao wa Jimbo.

Michango mikubwa ya fedha ya Serikali Kuu imewezesha shule kupata vyumba vinne (4) vya madarasa, vingine vinne (4) vinaendelea kujengwa. Ipo ofisi moja (1) ya walimu, na vyoo vyenye matundu 10 ya wanafunzi na 2 ya walimu.

Miradi ya Elimu Jimboni mwetu

Kwa wakati huu miradi ya elimu inayotekelezwa na Wanavijiji kwa kushirikiana na Serikali yetu, na Mbunge wa Jimbo ni:

(i) ujenzi wa sekondari mpya nne (4) zitakazofunguliwa mwakani (2024)

(ii) ujenzi wa maabara za masomo ya sayansi kwenye sekondari zetu zote za kata (Sekondari 25). Sekondari mpya zinazojengwa lazima ziwe na maabara.

(iii) ujenzi na upanuzi wa shule shikizi mpya na zilizosimamisha ujenzi
ELIMU ni kipaumbele cha kwanza cha Musoma Vijijini, tuendelee kuchangia miradi yetu ya elimu tukiwa tunajitayarisha kutekeleza sera mpya ya elimu na mitaala yake.

Halmashauri yetu (Musoma DC) inaombwa nayo ianze kuchangia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya wananchi wa Musoma Vijijini.*

Picha za hapa juu ni ujenzi wa Shule Shikizi Kiunda inayojengwa kwenye Kitongoji cha Kiunda, Kijijini Kamguruki, Kata ya Nyakatende, Musoma Vijijini.

Imetolewa na, 
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news