Serikali yafunga Uwanja wa Benjamin Mkapa na Uhuru jijini Dar es Salaam

DAR ES SALAAM-Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imeufungia Uwanja wa Benjamín Mkapa na Uhuru jijini Dar es Salaam Jijini Dar kwa ajili ya matengenezo hadi Oktoba mwaka 2024.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya wizara ambayo imetolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Aron Msigwa;

"Hata hivyo, kutokana na maombi ya timu zinazocheza Ligi Kuu na uhitaji mkubwa wa viwanja hivyo kwa ajili ya michuano ya Kimataifa, wizara iliridhia ombi la kuendelea kutumika kwa viwanja hivyo wakati ukarabati ukiendelea, kazi ya ukarabati mkubwa inaendelea katika Uwanja wa Benjamin Mkapa na ukarabati mkubwa wa Uwanja wa Uhuru upo mbioni kuanza baada ya taratibu za kumpata mkandarasi kukamilika.

“Kwa kuwa ni muhimu kuzingatia kanuni zinazosimamia Ligi Kuu na michuano ya Kimataifa, wizara inatangaza kuvifunga viwanja vya Benjamin Mkapa na Uhuru mpaka hapo ukarabati utakapokamilika Oktoba, 2024.

"Kwa taarifa hii timu zilizoomba kutumia viwanja hivi kama viwanja vyao vya nyumbani zinajulishwa kutafuta viwanja vingine, Wizara inaomba radhi kwa usumbufu wowote ambao wanamichezo wataupata kutokana na kufungwa kwa viwanja hivi;

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news