Simba Queens yatinga fainali ya Ngao ya Jamii kwa kuichakaza Yanga Princess

DAR ES SALAAM-Kikosi cha Simba Queens kimetinga fainali ya Ngao ya Jamii baada ya kuifunga Yanga Princess kwa mikwaju ya penati 5-4 katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Azam Complex Chamazi.

Mchezo huo ambao Simba Queens waliutawala sehemu kubwa ulimalizika kwa sare ya bila kufungana huku wachezaji wao wakipoteza nafasi nyingi za wazi.

Kama wachezaji hao wangeongeza umakini katika nafasi walizotengeneza walikuwa na uwezo wa kuimaliza mechi ndani ya dakika 90.

Kocha Mkuu, Juma Mgunda alifanya mabadiliko ya kuwatoa Joanitha Ainembabazi na Elizabeth Mutukiza na kuwaingiza Aisha Juma na Esther Mayala.

Penati zetu zote tano zilifungwa na Esther Mayala, Aisha Juma, Mwanahamis Omary, Ruth Ingosi na Vivian Corazone.

Queens itakutana na JKT Queens iliyoifunga Fountain Gate kwa mabao 5-0 katika mchezo wa fainali utakaopigwa Disemba 12 katika Uwanja wa Azam Complex.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news