DAR ES SALAAM-Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk amekutana kwa mazungumzo na Rais wa Taasisi ya Waturuki waishio Nje ya Uturuki na Jamii zao (YTB), Bw. Abdullah Eren katika ofisi ndogo za wizara jijini Dar es Salaam.

Amesema,uhusiano kati ya Tanzania na Uturuki ni wa muda mrefu na unaoongoza hasa katika sekta za elimu, afya, biashara na uwekezaji na kuelezea matumaini yake kuwa uhusiano huo utaendelea kuimarika zaidi.





Balozi wa Saudi Arabia nchini, Mhe. Yahya Ahmed Okesh akimkabidhi ujumbe maalum kwa Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.