Tanzania yasaini mkataba mpya wa ubia na nchi za OACPS na EU



Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji, Luxembourg na Mwakilishi kwenye Umoja wa Ulaya na Jumuiya ya Nchi za Afrika, Caribbean na Pacific (OACPS) Mhe. Jestas Abuok Nyamanga, akisaini kwa niaba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mkataba Mpya wa Ubia baina ya Nchi za OACPS na Umoja wa Ulaya (Mkataba wa Samoa). Hafla ya kusaini Mkataba huo ilfanyika tarehe 19 Desemba 2023 katika Makao Makuu ya OACPS Brussels Ubelgiji. Wanaoshuhudia tukio hilo ni maafisa waandamizi kutoka Sekretarieti ya OACPS na Umoja wa Ulaya.

Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji, Luxembourg na Mwakilishi kwenye Umoja wa Ulaya na Jumuiya ya Nchi za Afrika, Caribbean na Pacific (OACPS) Mhe. Jestas Abuok Nyamanga, akisaini kwa niaba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mkataba Mpya wa Ubia baina ya Nchi za OACPS na Umoja wa Ulaya (Mkataba wa Samoa).
Mhe. Balozi Jestas Abuok Nyamanga (katikati) ameshika Mkataba Mpya wa Ubia baina ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika, Caribbean na Pacific (OACPS) na Umoja wa Ulaya baada ya kusainiwa katika hafla fupi iliyofanyika Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Caribbean na Pacific, jijini Brussels Ubelgiji tarehe 19 Desemba 2023. Waliosimama pamoja naye ni wawakilishi kutoka Umoja wa Ulaya na OACPS.
Kaimu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Afrika, Caribbean na Pacific (OACPS) Dkt. Ibrahim Richard akimpa mkono kumpongeza Mhe. Balozi Jestas Abuok Nyamanga baada ya kusaini mkataba huo kwa niaba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mhe.Balozi Jestas Abuok Nyamanga katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania, Brussels baada ya kusaini Mkataba Mpya wa Ubia baina ya Jumuiya ya Nchi za Afrika, Caribbean na Pacific (OACPS) na Umoja wa Ulaya katika hafla iliyofanyika katika Makao Makuu ya OACPS Brussels tarehe 19 Desemba 2023. Aliyesimama kulia kwa Balozi Nyamanga ni Dkt. Ibrahim Richard Kaimu Katibu Mkuu wa OACPS.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news