"Nimesikitishwa na kifo cha Ndugu Joseph Sebastian Pande, aliyekuwa akitumikia nchi yetu katika nafasi ya Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka.
"Nawapa pole Mkurugenzi wa Mashtaka, Ndugu Sylvester Mwakitalu, familia, wakuu wa divisheni na vitengo, wafanyakazi wote katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka, ndugu, jamaa na marafiki. Mwenyezi Mungu aiweke roho yake mahali pema. Amina,"ameeleza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Samia Suluhu Hassan kupitia WhatsApp yake leo Desemba 20,2023.
Tags
Habari
Mkurugenzi wa Mashtaka nchini
Ofisi ya Taifa ya Mashtaka
Tanzania
Wakili Mkuu wa Serikali