Ufaransa yampa heshima Mtanzania Rhobi Samwelly

NA DIRAMAKINI

MKURUGENZI wa Shirika la Hope for Girls and Women in Tanzania (HGWT) linalojishughulisha na mapambano ya vitendo vya ukatili wa kijinsia mkoani Mara, Rhobi Samwelly amepata heshima ya kualikwa na Serikali ya Ufaransa kuhudhuria warsha inayohusu masuala ya haki za binadamu na maendeleo.
Mchango na juhudi za Rhobi Samwelly katika kutetea haki za wanawake na watoto nchini Tanzania, zimeendelea kuthaminiwa na Serikali ya Ufaransa na aliweza kutunukiwa tuzo ambayo hutolewa na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ya 'Marianne Initiative' ambayo hutolewa kwa watetezi wa haki za binadamu wanaofanya vizuri sana katika mataifa yao.
Akizungumza na DIRAMAKINI akiwa nchini Ufaransa leo Desemba 11, 2023, Rhobi amesema kuwa, ni faraja kubwa kwake kuona juhudi na mchango weke unathaminiwa. Kwani kupitia warsha hiyo amepata fursa ya kuzungumza na Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron.
Amesema, ataendelea kuwa mstari wa mbele kutetea haki za binadamu yakiwemo masuala yanayowahusu wanawake na watoto nchini Tanzania pamoja na Maendeleo na kuwa na ari na nguvu mpya ya kufanya majukumu hayo kwa ufanisi.
"Nashukuru kupata mwaliko kutoka serikali ya Ufaransa kuhudhuria warsha inayohusu masuala ya haki za binadamu pamoja na Maendeleo, ni warsha ambayo imekuwepo toka jumatano hadi Decemba 10, 2023, ambapo watetezi wa haki za binadamu kutoka mataifa mbalimbali tumekutana na kuhitimishwa na hotuba ya Rais Emmanuel Macron," amesema Rhobi na kuongeza kuwa.
"Niseme tu kwamba nitaendelea kushiriki vyema katika kutetea haki za binadamu katika nchi yangu nikishirikiana na serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa kielelezo bora kitaifa na Kimataifa kuona wanawake na watoto wanakuwa na ustawi bora,"amesema Rhobi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news