Uholanzi kuijengea Muhimbili uwezo zaidi kwenye upasuaji wa taya na uso

DAR ES SALAAM-Taasisi ya Watalaam wa Upasuaji Uso na Taya ya nchini Uholanzi (Dutch Foundation for Oral Maxillofacial) imeahidi kushirikiana na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) katika kuwajengea uwezo zaidi watalaam wa fani hiyo ili kuongeza wigo na kuwafikia wananchi wengi wenye uhitaji wa huduma hiyo nchini.
Hayo yamesemwa leo na Mjumbe wa Bodi ya taasisi hiyo, Dkt. Albert Wittkampf alipomtembelea Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Prof. Mohamed Janabi ili kuona fursa ya ushirikiano katika eneo hilo.

Prof. Janabi amemueleza kuwa moja ya jambo muhimu kwa watalaam ni kuwapa ujuzi ambao unalingana na mabadiliko ya teknolojia ya utoaji huduma na matumizi ya vifaa tiba vya kisasa vilivyopo duniani.

Tanzania ina Madaktari Bingwa wa Upasuaji Taya na Uso 26 ambapo 16 kato yao wanapatikana eneo la MNH.

Ushirikiano huu unategemea kuanza mapema mwakani ambapo timu ya watalaam kutoka Uholanzi watakuja kushirikiana na wenzao wa MNH ili kujenga uwezo katika maeneo ambayo wana upungufu wa ujuzi na vifaa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news