MARA-Jimbo la Musoma Vijijini limeamua kutatua tatizo sugu la ukosefu wa maabara za masomo ya sayansi kwenye sekondari zake za kata.
Lengo kuu:
Kila Sekondari ya Kata ipate maabara nzuri na za kisasa za masomo matatu ya sayansi - physics, chemistry & biology labs.
Wachangiaji wakuu wa mradi huu ni:
1. Wanavijiji
2. Serikali Kuu
3. Mbunge wa Jimbo
4. Mfuko wa Jimbo
5. Baadhi ya wazaliwa wa Musoma Vijijini
Halmashauri yetu (Musoma DC) inaendelea kushauriwa nayo ianze kuchangia mradi huu kwa kutumia mapato yake ya ndani!
Takwimu za maabara tulizonazo:
(A) Sekondari zenye maabara tatu (3):
1. Bugwema 2. Kiriba
3. Ifulifu 4. Mugango
5. Bwai (zinakamilishwa Jan 2024)
(B) Sekondari zenye maabara mbili (2):
6. Bulinga 7. Kigera
8. Nyakatende 9. Makojo
10. Nyambono 11. Nyegina
11. Rusoli 13. Suguti
(C) Sekondari zenye maabara moja (1):
14. Bukima 15. Dan Mapigano (Bugoji)
16. Etaro 17. Kasoma18. Mabuimerafuru
(D) Sekondari zizokuwa na maabara hata moja
19. Nyegina 20. Busambara
21. Mtiro 22. Murangi
23. Nyanja 24. Seka
25. Tegeruka
Sekondari za binafsi zimejenga maabara zake
26. Bwasi (Kanisa la Wasabato/SDA)
27. Nyegina (Kanisa Katoliki/RC)
Karibuni tuendelee kuchangia ujenzi wa maabara za masomo ya sayansi kwenye sekondari zetu za kata za Musoma Vijijini
Tafadhali sana usisahau harambee ya ujenzi wa maabara za Etaro Sekondari utakaofanyika Ijumaa, 15.12.2023 (tangazo la harambee linatolewa leo)
Sayansi ni kila kitu
&
*Kila kitu ni Sayansi
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijiniwww.musomavijijini.or.tz