Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akizungumza na kaka yake Padre Sebastian Mpango (kushoto) pamoja na Padre Emmanuel Mtambo (kulia) mara baada ya kushiriki Ibada ya Jumapili katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowska Kiwanja cha Ndege Dodoma leo tarehe 10 Desemba 2023.
“Asanteni sana kwa kuniombea, yamesemwa mengi si ndio?Na wengine bado wanasema mimi ni mzuka, mnaopenda kusoma Biblia labda niwakumbushe sehemu moja halafu mtamalizia Zaburi ya 118 aya ya 17 inasema ‘Sitokufa bali nitaishi, nami nitayasimulia matendo ya Bwana’ kwahiyo mkae na amani nipo salama nilikwenda nje kufanya shughuli kwa mwezi mmoja, sijapungua hata kidogo,"Makamu wa Rais, Dkt.Philip Mpango.