Viongozi wa umma wapewa siku 10 kuwasilisha tamko la rasilimali na madeni

DODOMA-Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma imewataka viongozi wote wa umma kuzingatia matakwa ya Katiba na Sheria ya Maadili.
Ni kwa kuwasilisha tamko la rasilimali na madeni ifikapo Desemba 31,2023.

Katibu, Ukuzaji wa Maadili,Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma,Waziri Kipacha ameyasema hayo Desemba 21,2023 jijini Dodoma wakati akizungumza na Wanahabari.

Amesema kuwa, mwenendo wa uwasilishaji taarifa hizo hauridhishi kwani hadi kufikia Desemba 20,2023 ni viongozi 2,475 pekee ndio wameweza kuwasilisha tamko lao kwa Kamishna wa Maadili.

Idadi ikiwa ni ndogo kati ya viongozi 15,762 sawa na asilimia 16 ya viongozi wote huku zikiwa zimebaki siku 10 kufika tarehe ya mwisho.

"Napenda kuchukua nafasi hii kuwaomba ambao bado watimize wajibu wao ili kuungana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hasan, Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango na Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa ambao tayari wametimiza wajibu huo, “amesema Kipacha.

Vile vile, amewataka viongozi wengine ambao bado hawajawasilisha matamko yao wakiwemo waliotamkwa katika tangazo la Serikali Na. 857 la Novemba 24,2023 kuwa tangu siku ya tangazo hilo wanawajibika kutimiza masharti yote ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Amesema,taarifa zinazotakiwa kutumwa na viongozi ni pamoja na majina matatu, simu ya mkononi, barua pepe binafsi ya kiongozi husika, taasisi anayofanyia kazi wadhifa wa kiongozi na tarehe ya uteuzi.

Pia, akizungumzia kuhusu viongozi wapya amesema watatatikiwa kuwasilisha taarifa zao ndani ya siku 14 baada ya kuteuliwa au kupandishwa cheo ambapo watatumiwa taarifa za siri kwa ujumbe mfupi kupitia simu zao kuwezesha kuingia kwenye mfumo wa Hifadhi ya Data ya Uendeshaji (ODS).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news