MBEYA-Wakaguzi wa kata nane wa Mkoa wa Mbeya wamekabidhiwa pikipiki aina ya Boxer kwa ajili ya kurahisisha na kufanikisha utekelezaji wa majukumu yao katika kata zao.
Akizungumza wakati wa kukabidhi pikipiki hizo katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika Desemba 2, 2023 katika uwanja wa FFU Mbeya, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, ACP Benjamin Kuzaga amemshukuru Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IJP Camillus Wambura kwa kutambua umuhimu wa vitendea kazi.