Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wapewa neno

MOROGORO-Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama ametoa wito kwa watumishi walio chini yake kufanya kazi kwa kutegemeana na kushirikiana bila kutengeneza makundi.
Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) wakisikiliza mkutano wa Baraza hilo uliofunguliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama.

Ametoa rai hiy Desemba 14, 2023 mkoani Morogoro wakati akifungua kikao cha Baraza la wafanyakazi la Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na uratibu kilicholenga kujadili Taarifa ya Bajeti ya 2023-2024 ya Ofisi hiyo.

Waziri Mhagama alisema, kuna kila sababu ya kufanya maamuzi ya pamoja ya ushirikishwaji ili kuweza kupata mafanikio kwenye idara na vitengo, kama viongozi wenu wanavyofanya kazi vizuri kwa kushirikiana.

Aliendelea kusema kuwa, hata kama inafikia wakati Mtendaji hayupo kwenye Idara au kitengo kuwe kuna Mtu anayeweza kufanya kazi kwa viwango na uwezo huo huo ili mambo yaweze kwenda vizuri.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza wakati akifungua mkutano wa Baraza la Wafanyakazi katika ofisi yake uliofunguliwa Desemba 14,2023 mkoani Morogoro.

“Tukifanya kazi kwa umoja na ushirikiano tukifanikiwa tuwe tumefanikiwa wote na tukianguka tujue tumeanguka wote na tujipange ili kujua sababu ya kuanguka na tuweze kujipanga,"alibainisha.

Aidha, Waziri Mhagama alisema anafarijika na utendaji wa kitaasisi na kuwaomba watumishi kuendelea kuimarisha utendaji wa kitaasisi ambao unatoa fursa kwa kila mtu kuwa ni sehemu ya mafanikio na ufanisi wa taasisi.

“Wale ambao Mnamadaraka kwenye Idara Vitengo au Taasisi zetu Muhakikishe Mnajenga moyo wa kukuza watumishi walio chini yenu, kwa kuwapa fursa ya kukua kielimu ndani ya ofisi, kukua kiujuzi na kukua kiubobezi,"alihimiza.
Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) wakisikiliza mkutano wa Baraza hilo uliofunguliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama.

Alibainisha kuwa Watumishi wa umma ni rasilimali muhimu, ya kuendesha rasilimali nyingine na kusema kuwa ni lazima tuiratibu vizuri Rasilimali hiyi na kuilinda kwa nguvu zote ili kuweza kupata mafanikio tuliyoyakusudia.

Waziri alisema; "Rais wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin Mkapa aliwahi kusema,” jambo muhimu kwa mfanyakazi si muda anaotumia kufanya kazi,bali kiasi cha kazi anachoweza kufanya katika muda aliopewa."

Alisema, Kuna kila sababu ya kuanzaa kujipima wenyewe hasa katika kuelekea kuanza mwaka 2024, ili kujua kiasi cha kazi tuliyoifanya na ufanisi wake kila siku anayoshiriki kama mtumishi wa umma katika ofisi ya waziri Mkuu.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Dkt. Jim Yonazi amesema, vikao vya wafanyakazi ni tamko la kisheria ambalo chimbuko lake ni Hayati Baba wa Taifa mwalimu Julius Nyerere, Rais wa awamu ya Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alilolitoa katika tamko no 1 la mwaka 1970 linalohimiza ushirikishwaji kupitia Baraza la wafanyakazi.

"Baraza ni kiungo muhimu kati ya wafanyakazi na Menejimenti na Ofisi ya Waziri Mkuu, tutaendele kuwa vikao hivi vya baraza la wafanyakazi kwa mujibu ya miongozo.
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri MKUU (Sera, Bunge na Uratibu) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa ofisi hiyo wakiongozwa na Waziri wa Nchi katika ofisi hiyo Mhe. Jenista Mhagama mara baada ya kufungua mkutano.

Awali akitoa salamu Katibu wa TUGHE Mkoa wa Dodoma Bw. Samwel Nyungwa ameipongeza Menejimenti ya Ofisi ya Maziri Mkuu, kwa kutekele za Sera ya ushrikishwaji kikamilifu,

Chama cha wafanyakazi kinaamini hakuna haki bila wajibu, tunaangalia namna tunavyopata haki na namna ambavyo tunatekeleza wajibu katika kuhakikisha mipango iliyopangwa inakamilika sawasawa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news