Charles Kulwa Memorial Hospital yawapima wazee magonjwa yasiyoambukiza bure

GEITA-Hospitali ya Kumbukumbu ya Charles Kulwa iliyoko wilayani Bukombe inaendesha zoezi la kufanya vipimo vya kuchunguza bure magonjwa matatu yasiyo ambukiza kwa wazee wenye umri kuanzia miaka 50 na kuendelea.
Mkurugenzi wa Hospitali hiyo Dkt.Baraka Charles amesema kuwa kufika Novemba 30,2023 wazee waliokuwa wamejitokeza kujiandikisha kwa ajili ya kufanyiwa vipimo ni 600.

Amesema magonjwa yatakayo chunguzwa ni kisukari, Moyo pamoja na tezi dume kwa wanaume.
Dkt. Charles amesema huduma hiyo inatolewa bure ikiwa ni huduma kwa jamii lakini pia kuzuia vifo ambavyo vinazuilika ambavyo vinaweza kusababishwa na magonjwa hayo.

Hata hivyo amefafanua kuwa zoezi hilo limeanza mwisho wa mwaka huu lakini litafanyika tena mwanzo wa mwaka kesho na litakuwa linafanyika kila miezi mitatu.

Mkuu wa Wilaya ya Bukombe, Said Nkumba ameipongeza Hospitali hiyo kwa kuamua kuhudumia bure kundi hilo la watu wazima ambalo limeonekana linakabiliwa sana na magonjwa hayo kuliko makundi mengine.

Akisoma risala mbele ya mgeni rasmi ambaye alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Bukombe, Said Nkumba, Dkt . Victor Kuyumba amesema kuwa Hospitali hiyo imeamua kuchagua kundi hilo la wazee kwasababu ndilo liko kwenye hatari kupata madhara endapo uchunguzi hautafanyika mapema.
Aidha,ameeleza kuwa Hospitali hiyo imefanikiwa kuongeza vifaa vya kisasa vya upasuaji na kuimarisha huduma ya kichwa na meno kwa kuongeza vifaa .

Ameeleza kuwa, hospitali inatoa huduma za kibingwa ambapo wana madaktari bingwa wa Moyo, bingwa wa Mifupa, Bingwa wa upasuaji wa jumla, Bingwa wa akina mama na Daktari Bingwa wa upasuaji wa Masikio na koo.
Baadhi ya wazee waliojitokeza kufanyiwa uchunguzi wameipongeza Hospitali hiyo kutoa huduma hiyo bure kwao kwani baadhi ya wazee hawana kipato cha kulipia vitimo na dawa.

Mzee Francis Banyikwa amesema kuwa Uongozi wa Hospitali hiyo umefanya uamuzi mzuri kuchagua kutoa huduma kwa wazee kwa sababu wengi wao hawajiwezi kiuchumi.
Zoezi hilo limezinduliwa Novemba 30,2023 na Mkuuwa Wilaya ya Bukombe Said Nkumba na litaendelea hadi Desemba 1,2024.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news