DAR ES SALAAM-Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA Council of Ministers) kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia Desemba 7, 2023.

Mkutano huo chini ya Uenyekiti wa Waziri Dkt.Kijaji umepitisha Itifaki ya AfCFTA ya Wanawake na Vijana katika Biashara ambayo imekamilika chini ya usimamizi wa Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri na Muungano wa Tanzania na Mhamasishaji Mkuu na Kinara wa Wanawake na Vijana katika Biashara Barani Afrika.