Waziri Silaa:Msinunue ardhi kwa fedha taslimu

TANGA-Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Jerry Silaa ametahadharisha wananchi kutofanya mauziano na manunuzi ya ardhi kwa fedha taslimu ili kuepuka utapeli.
Waziri Silaa ametoa tahadhari hiyo mkoani Tanga wakati alipofanya ziara ya kufuatilia maelekezo ya Baraza la Mawaziri kuhusu migogoro ya vijiji 975 nchini.

Onyo hilo la Waziri Silaa limekuja baada ya kukutana na malalamiko mengi ya wananchi yanayokuja kwake kama migogoro ya ardhi chanzo kikuu ni mauziano yasiyo na ushahidi wa miamala.

Amesema, ni vyema mauziano ya ardhi yafanyike kwa miamala ya Benki au miamala ya Simu ili kuwa na ushahidi wa mauziano ya ardhi kwani nchi yetu kwa sasa imeendelea katika teknolojia ya miamala ya Benki na Simu hivyo haina haja ya kufanya malipo kwa fedha taslimu.

Aidha, amesema Wizara ya Ardhi kwa sasa imejipanga kuboresha mifumo ya TEHAMA ili kuongeza kasi ya miamala ya ardhi, kuondoa usumbufu na kuchangia katika uchumi wa nchi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news