Waziri Ummy akemea vikwazo vya huduma kwa wajawazito wasioambatana na wenza kliniki

TANGA-Waziri wa Afya Mhe. Ummy mwalimu ametaka kutowekewa vikwazo kwa mama mjamzito pindi anapoenda kliniki ya mama na mtoto bila ya kuwa na mwenza wake.
Waziri Ummy amesema hayo Novemba 30, 2023 kwenye Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia yaliyofanyika katika Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga.

“Tusiweke vikwazo kwa wanawake ambao wamepata ujauzito na wanaenda kliniki bila ya wenza wao kupata huduma, tuwashauri na tuwape elimu ili waende na wake zao lakini tusiwanyime huduma sababu hawakwenda na wenza wao,”amesema Waziri Ummy.

Amesema, wanawake wengi wanapewa ujauzito na wanaachwa na wanaume wakihangaika peke yao l, utamlazimisha vipi aende na mwanaume wakati amemuacha.

Waziri Ummy amepiga marufuku kulazimisha mwanamke mjamzito kwenda na mwenza wake kliniki ili kupata huduma.

“Hii imepelekea wanawake wanatafuta bodaboda au mwanaume yeyote ampeleke kliniki ili apate huduma hii haikubaliki,” amesema Waziri Ummy

Amesema, inapaswa wanaume wahamasishwe, wapewe elimu kuwa hili ni muhimu baba na mama wote wakaenda kwa pamoja wakaenda kliniki lakini sio kuwalazimisha wanawake.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news