Young Africans SC yaichapa Medeama SC mabao 3-0

DAR ES SALAAM-Klabu ya Young Africans (Yanga SC) imetwaa alama tatu katika mchezo muhimu wa Klabu Bingwa barani Afrika dhidi ya Medeama SC kutoka Tarkwa nchini Ghana.

Ni kupitia mtanange ambao umepigwa Desemba 20,2023 katika Dimba la Benjamin Mkapa lililopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Mabingwa hao wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara wamepata ushindi wa wa mabao 3-0 ambapo mchezo huo ulikuwa na umuhimu kuelekea kufuzu robo fainali ya michuano hiyo mikubwa Afrika.

Dakika ya 33 ya mtanange huo kiungo Pacome Zouzou alianza kuwapa raha waajiri wao kwa bao safi ambalo lilionekana neema kwa kipindi chote cha kwanza.

Licha ya Medeama SC kupata fursa ya mkwaju wa penati mara baada ya mshambuliaji wao Sowah kuchezewa rafu na mlinzi wa Yanga, Bakari Nondo Mwamnyeto mlinda mlango wa Yanga SC, Djidji Diara alifanikiwa kuzima ndoto hiyo.

Dakika ya 61 Bakari Nondo Mwamnyeto alitupia bao la pili, hivyo kuwafanya waajiri wake Yanga SC kuendelea kuwa na akiba nzuri ya mabao.

Aidha, Mudathir Yahya dakika ya 66 alizima kabisa ndoto ya Medeama SC kusonga mbele kwa mabao baada ya kupachika bao la tatu ambalo lilikuwa ni funga kazi.

Katika kundi D hilo,Yanga SC inashika nafasi ya pili huku ya kwanza ikishikiliwa na Al Alhly kutoka Misri, nafasi ya tatu inachukuliwa na Chabab Riadhi Belouizdad au CR Belouizdad kutoka ncjhini Algeria huku Medeama SC wakiburuza mkia.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news