Young Africans yatoa sare ya 1-1 na Medeama SC jijini Kumasi

KUMASI-Penalti ya dakika ya 27 iliyotumbukizwa katika nyavu za Young Africans (Yanga SC) ya jijini Dar es Salaam na kiungo wa Medeama SC, Jonathan Sowah iliwafanya mashabiki na wachezaji wa klabu hiyo kuwa na msongo wa mawazo.

Lakini, ndani ya kipindi hicho hicho cha kwanza,kiungo Pacome Zouazoua katika dakika ya 36 alirejesha tabasamu la waajiri wake Yanga SC baada ya kusawazisha bao hilo.

Ni kupitia mtanange wa Kundi D wa Ligi ya Mabingwa barani Afrika ambao umechezwa Desemba 8,2023 katika Dimba la Baba Yara jijini Kumasi nchini Ghana.

Sare hiyo inazidi kurejesha matumaini kwa wawakilishi hao wa Tanzania kutinga hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika.

Vile vile, kupitia mtanange mwingine wa kundi hilo Al Ahly ya Misri imelazimishwa sare ya bila mabao na CR Belouizdad ya Algeria katika dimba la Borg El Arab jijini Alexandria, Misri.

Klabu ya Al Ahly inaendelea kuongoza Kundi D kwa alama tano ikifuatiwa na CR Belouizdad yenye alama nne sawa na Medeama wakati Yanga SC ina alama mbili tu.

Aidha, mitanange ijayo Desemba 20,2023, Klabu ya Yanga itawakaribisha Medeama SC katika Dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam huku Al Ahly wakiwa wageni wa CR Belouizdad tarehe 19, 2023 huko jijini Algiers.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news