ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema hakuna maendeleo pasipo na amani, umoja na mshikamano wa watu.
Rais Alhajj Dkt.Mwinyi amesema hayo Januari 5,2024 alipojumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika ibada ya sala ya Ijumaa Msikiti wa Riyadhu swalihin Wilaya ya Chakechake, Mkoa wa Kusini Pemba.
Aidha,Rais Dkt.Mwinyi amewataka waumini kuendelea kumuomba Mwenyezi Mungu kudumisha amani, upendo, umoja na mshikamano.
Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa ni wajibu kuwanasihi vijana kufanya kazi za halali na kuepuka kushiriki vitendo viovu.