ANGALIZO PICHA ZINATISHA: Mbwa aina ya Bull washambulia familia na kusababisha madhara huko Usagara

MWANZA-Usiku wa kuamkia Januari 8,2024 majira ya saa nne usiku familia ya Nicholaus Kunju ilishambuliwa na mbwa na kuisababishia madhara kwenye sehemu mbalimbali za miili yao.
Kwa mujibu wa mtoa taarifa walioshambuliwa ni mke wake pamoja na watoto. Tukio hilo linawahusisha mbwa wawili aina ya Bull Dog ambao anawafuga kwa ajili ya ulinzi nyumbani kwake Usagara.

Mbwa hao walimshambulia binti yake wakati ametoka nje usiku huo wa saa nne akiwa amesindikizwa na kaka yake, mara baada ya uvamizi huo kijana mwingine na mama yao walitoka kutoa msaada, lakini mbwa hawakuwatii na kuwashambulia wote.

"Wote walioshambuliwa na mbwa sio wageni kwa mbwa hao,kwani wamekuwa wakiwahudumia kwa chakula.

"Baada familia hiyo kujinusuru na kukimbilia ndani,mbwa waliendelea kuwa wakali na hapakuwa na uwezekano wa kuwapatia huduma majeruhi, kwani hakuna aliyeweza kuingia wala kutoka ndani ya uzio.
"Wakati haya yanatokea Kunju alikuwa kazini zamu ya usiku na alipigiwa simu kujulishwa juu ya tukio hilo na kuambiwa mmoja wa majeruhi ana hali mbaya.

"Tulibahatika kufanya mawasiliano na Polisi Kituo cha Misungwi ili waweze kufika eneo la tukio waue mbwa ili msaada kwa majeruhi upatikane.

"Kwa ushirikiano na Zombwe na Lenox tulifanikisha kumtoa Kunju kazini ili akashiriki uokoaji.

"Polisi walifika nyumbani kwa Kunju majira ya saa saba usiku wakitanguliwa na watu wa Maliasili na wafanikiwa kuwapiga risasi mbwa wote wawili na majeruhi wakapelekwa Hospilali ya CF kwa Matibabu.

"Majeruhi wote wanaendelea vizuri.Shukrani kwa wote walioshiriki kwenye utatuzi bila kumsahau Sheik Abdallah Omari.

"Hii aina ya mbwa sio ya kufuga kabisa. Ukifuatilia historia ya mbwa hawa ni mbaya sana.

"Wanaua sana wamiliki. Hawa huwa kuna kipindi wanakuwa na tatizo la mental disorder. Yaani kuchanganyikiwa.
"Na huwa wanakuwa hatari sana. Kwani kipindi hicho hawajali hata kama wewe ndiye unayempatiaga huduma ya chakula.

"Ikumbukwe kwamba mmbwa hawa ni pandikizi. Yaani mchanganyiko wa mnyama mwitu na mbwa wa kawaida. Sasa ndio jasiri haachi asili.

"Hawa hawa ndio waliombadilikia Mzee Kingunge Ngombare Mwiru wakamuua. Historia yao sio nzuri,mbwa angalau wa kufuga kidogo kwa ajili ya ulinzi ni aina ya GS."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news