DAR ES SALAAM-Bodi ya Sukari nchini Tanzania imetoa Amri ya Bei Elekezi ya Sukari nchini humo, ambapo kwa bei ya jumla, kiwango cha chini kinaanzia sh. 2,600 hadi sh. 2,900.
Aidha,bei ya reja reja kiwango cha chini kinaanzia sh. 2,700 hadi sh. 3,200. Amri hii ni kwa mikoa yote nchini.
Hatua hii, inafuatia kupanda kwa bei ya sukari hadi kkufikiaTsh.5,400 kwa kilo kutokana na kuadimika kwa bidhaa hiyo sokoni.
Serikali imesema kiwango cha uzalishaji kimeshuka kwa tani elfu moja kwa siku kutokana na mvua kubwa zinazoendelea nchini humo.