ZANZIBAR-Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar imetiliana saini Hati ya Mashirikiano na Wizara ya Maliasili na Bahari ya Jamhuri ya Watu wa China.
Makubakiano hayo yamesainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi, Aboud Hussein Jumbe na Naibu Waziri wa Wizara ya Maliasili na Bahari ya Jamhuri ya Watu wa China,Mhe. Dkt. Sun Shuxien.
Sekta zitakazohusika na makubakiana hayo ni pamoja na Sekta ya Uchumi wa Buluu ikiwemo Sayansi na Teknolojia ya Baharini, Uchunguzi wa Mazingira ya Bahari, utabiri wa ufuatiliaji na tathmini ya kujikinga na maafa ya majanga baharini.
Pia makubakiano hayo yatahusisha Utafiti wa Baharini, kujengea uwezo, uwekezaji, uhifadhi wa viumbe hai wa baharini na ulinzi wa mfumo wa ikolojia wa baharini, pamoja na maeneo mengine ya Uchumi wa Buluu.
Mbali na hayo Jamhuri ya Watu wa China pia itatoa fursa za ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wa Kizanzibari katika fani za Uchumi wa Buluu na Usimamizi wa bahari.