MWANZA-Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA) imeendesha mafunzo na kutoa elimu kwa watumishi wa Bandari ya Mwanza na Kanda ya Ziwa kwa ujumla kuhusu dawa za kulevya.
Dezdel Tumbu ambaye ni Afisa Elimu wa DCEA Kanda ya Ziwa amesema, wanafanya hivyo kwa sababu bandari ni sehemu ambazo wauzaji na wasafirishaji wa dawa za kulevya huwa wanapatumia mara nyingi.
"Wauzaji na wasafirishaji wa dawa za kulevya wanaingiza mizigo na kutoa mizigo yao kupitia bandari.
"Kwa hiyo tunaamini kabisa kwamba kwa kuwaelimisha na kuwajengea uwezo maofisa wa bandari watatusaidia katika kufanya ukaguzi.
"Lakini pia kutambua mizigo ambayo inaweza kuingia ambayo inahusishwa na dawa za kulevya ili tatizo hili la biashara ya dawa za kulevya na matumizi liweze kuisha,"amesema Tumbu;
Tags
DCEA
DCEA Tanzania
Habari
Kataa Dawa za Kulevya na Timiza Ndoto Zako
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA)