Dkt.Kipesha aongoza kikao cha pili cha Baraza la Wafanyakazi wa TEA

MOROGORO-Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) wamekutana na kufanya kikao cha pili cha baraza la pili wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu, Dkt. Erasmus Kipesha. Kikao hicho kimefanyika Januari 19, 2024 mjini Morogoro.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Dkt. Erasmus Kipesha katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa mamlaka hiyo mjini Morogoro.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao hicho,Mwenyekiti wa baraza hilo, Dkt. Kipesha amewapongeza Sekretarieti ya Baraza kwa maandalizi mazuri ya kikao hicho muhimu kwa ajili ya kupitia na kujadili masuala mbalimbali ya kiutumishi na utekelezaji wa majukumu ya mamlaka hiyo.
Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la TEA wakisikiliza na kufuatilia taarifa mbalimbali zikiwasilishwa katika kikao cha pili cha baraza hilo kilichofanyika mjini Morogoro.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Dkt. Erasmus Kipesha (katikati) akisikiliza na kufuatilia taarifa mbalimbali katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi kilichofanyika mjini Morogoro. Kushoto ni Katibu wa baraza hilo kutoka TEA,Aidan Lucas.

Aidha, akiwasilisha taarifa ya mamlaka kwa wajumbe wa baraza hilo amesisitiza kuwa, ili TEA iweze kufikia malengo hasa ya kutekeleza miradi kwa ufanisi ni lazima utafutaji wa rasilimali upewe kipaumbele na kila mtumishi.

"TEA ilianzishwa kwa Sheria ya Mfuko wa Elimu na jukumu kuu la mfuko huo ni kutafuta rasilimali fedha kutoka kwa wadau mbalimbali wa masuala ya elimu ili kufadhili ujenzi wa miundombinu ya elimu,"amesema Dkt. Kipesha.
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la wafanyakazi la TEA wakisikiliza na kufuatilia taarifa mbalimbali zikiwasilishwa katika kikao cha pili cha Baraza hilo kilichofanyika mjini Morogoro.
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la wafanyakazi la TEA wakisikiliza na kufuatilia taarifa mbalimbali zikiwasilishwa katika kikao cha pili cha Baraza hilo kilichofanyika mjini Morogoro.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Dkt. Erasmus Kipesha akifafanua jambo katika kikao cha pili cha Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka hiyo kilichofanyika mjini Morogoro.
Mwakilishi kutoka Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi ya Elimu ya Juu Tanzania (THTU) Taifa Bi. Salma Fundi, akiwasilisha salamu kutoka makao makuu ya chama hicho kwa wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa TEA.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Dkt. Erasmus Kipesha akizungumza na wajumbe wa Baraza la wafanyakazi alipokuwa akifungua kikao cha pili cha Baraza la wafanyakazi wa Mamlaka hiyo mjini Morogoro.

Ameongeza kuwa, utekelezaji wa jukumu hilo siyo la mtu ama idara moja ndani ya mamlaka, bali ni wajibu wa kila mtumishi kutafuta vyanzo mbalimbali vya mapato ili kufikia malengo yaliyowekwa.

Wajumbe wa baraza walipokea taarifa hiyo ya Mkurugenzi Mkuu, wakaijadili na kuahidi kushirikiana kwa pamoja kutafuta wafadhili na wachangiaji wa elimu kupitia Mfuko wa Elimu wa Taifa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news