PWANI-Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi . Dkt. Moses Kusiluka amesema,Serikali itaendelea kutoa ushirikiano katika ujenzi wa Mradi Mkubwa wa Viwanda zaidi ya 200 unaoendelea kutekelezwa katika eneo la Kwala Kibaha mkoani Pwani.
Katibu Mkuu Kiongozi Kusiluka ameyasema hayo Januari 5,2024 akiongozana na Mawaziri na Wakuu wa Taasisi mbalimbali katika ziara
ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Mradi huo unaotarajiwa kuwa na viwanda zaidi ya 200 uliopo katika eneo la Kwala mkoani Pwani.
Amesema, Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan inaunga mkono jitihada zinazofanywa na wawekezaji na itahakikisha
Mradi huo muhimu na wenye faida nyingi hususani katika kuongeza ajira, Pato la Taifa na ukuaji wa uchumi wa Taifa kwa ujumla unakamilika.
Kwa upande wa Waziri wa Viwanda na Biashara Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt. Ashatu Kijaji ameseam Mradi huu unaojumuisha viwanda zaidi ya 200 utakapokamilika utatoa ajira zaidi ya laki moja na vijana wengi kutoka ndani ya Mkoa wa Pwani na Taifa kwa ujumla watapata ajira hali itakayoimarisha uchumi wa Taifa kwa ujumla
"Zaidi ya asilimia 90 ya mabinti ambao tuliowaona katika kile kiwanda cha kutengeneza nguo wanatoka hapa Kwala na waliniambia kabisa kuwa walitembea mitaani kwetu na kuweza kuwachukua wadada kila aliekuwa na cherehani yake nyumbani na kuanza nao hapa na wengine wanakuja," amesema Kijaji.
Aidha, Dkt.Kijaji alibainisha kuwa, katika ziara hiyo walitembelea viwanda viwili kati ya 200 na kimoja wapo ni cha kutengeneza nguo (vijora) zinatumika ndani ya Tanzania na vinasambazwa Dubai ambapo bidhaa hizo zinachangia upatikanaji wa fedha za kigeni kutokana na uwekezaji unaoendelea.
Tags
Bandari Kavu Kwala
Habari
Kongani ya Viwanda Kwala
Kwala Dry Port
Pwani Region
Wizara ya Viwanda na Biashara