Dkt.Slaa acha chuki binafsi kwa Rais Dkt.Samia wakati Magufuli akitoa sadaka makanisani ulifunga mdomo-Mwinjilisti Temba

NA DIRAMAKINI

MUHUBIRI na Mwinjilisti wa Kimataifa, Alphonce Temba amemtaka mwanasiasa na padri mstaafu Dkt.Wilbroad Slaa kuacha chuki binafsi dhidi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Amesema, kauli za mwanasiasa huyo kupiti Clubhouse, mtandao ambao umejumuisha Watanzania wengi kutoka ndani na nje ya nchi kuhusu sadaka anazotoa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia kwa ajili ya kujenga makanisa hazina afya.

Ni baada ya mwanasiasa Dkt.Wilbroad Slaa kuonekana kukesha katika mtandao huo kila siku kuilaumu Serikali na yale ambayo yanafanywa na Rais Dkt.Samia.

"Pamoja na mambo mengi mazuri ambayo Dkt.Slaa anayafanya kwa manufaa mbalimbali ya nchi, lakini inaonekana kabisa Dkt.Slaa kuwa na chuki binafsi na Rais wa Serikali ya Awamu ya Sita ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan,"amesema Mwinjilisti Temba.

Kutokana na hali hiyo, Mwinjilisti Temba amemtaka Dkt.Slaa kurejea wito wake wa kipadri na misingi aliyoisomea ya utumishi wa Mungu ya umoja, amani na upendo na mshikamano.

"Kama ni jambo la msingi bila kujalisha masuala mengine ya kiitifaki ya kisiasa, kijamii na yeyote yanayoendelea. Ikumbukwe kuwa Mheshimiwa Freeman Mbowe ni mwanadamu, Mheshimiwa Rais Dkt.Samia ni mwanadamu.

"Na, kwa mazingira ya maisha ya kibinadamu kuna maeneo watakuwa hawakubaliani kabisa, hata kwa kupelekana mahakamani, lakini kuna maeneo lazima wanatakiwa waunganishwe na kukubaliana kwa sababu moja tu.

"Nayo ni maeneo ya Kiroho,kama Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ametoa shilingi milioni 150 kwa ajili ya huduma za kiroho, ijulikane kwamba, Samia Suluhu Hassan ni Muislamu na ni Rais wa nchi.

"Nilitegemea kusikia kelele za kupinga na kulalamika zitoke kwa jamii ya Waislamu, Mashehe na Mufti wa BAKWATA kwa nini alifanya jambo hilo.

"Kitendo cha viongozi wake kutokupiga kelele kusaidia huduma za ujenzi wa Kanisa na kitendo cha Dkt.Slaa ambaye ni padri mstaafu, aliyekuwa padri aliyejiuzulu kuendelea kupinga huduma za kiroho kuendelea kusaidiwa na Mama Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,

"Na akaendelea kukiri kwamba huko msaada uliotolewa katika jimbo lake, Kanisa Katoliki akahudhuria bila shaka wa shilingi milioni 100 na anapinga hizo fedha zinatoka wapi ama za Rais ama za Ikulu ni chuki binafsi.

"Jambo ambalo ni suala la kibinafsi hutoaji wa fedha hizo, ni suala la kibinafsi huenda Rais Dkt.Samia pamoja na marafiki zake wameamua kuchanga fedha hizo na kuzitoa kwa ajili ya kazi za huduma za kiroho.

"Na kupinga pia msaada uliotoka kwa mtumishi wa Mungu, Mtume Mwanposa kutoka Kawe jijini Dar es Salaam zikiwakilishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

"Kwamba fedha hizo zinazotoka kwa Rais zinatokatokaje, kwa nini wananchi wasiingilie taratibu hizo.

"Nashindwa kumuelewa Dkt.Slaa ambaye ni kiongozi wa kiroho na amewahi kuwa Balozi na Mbunge na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

"Sikutegemea kabisa kwa nafasi alizozishika na elimu aliyonayo kuirudisha nchi katika giza.

"Ina maana Balozi Slaa ambaye amefanya kazi za kibalozi, amekuwa chini ya Rais wa Awamu ya Tano, Hayati Dkt.John Pombe Joseph Magufuli kasahau kuwa, kanisa la GRC la Mzee wa Upako, Anthony Lusekelo lililopo Ubungo Kibangu, Hayati Dkt.Magufuli aliwahi kutoa sadaka kanisani pale akiwa na mkewe.

"Na kuahidi kutengeneza barabara ya lami mpaka hapo kanisani, barabara ambayo haikuwa katika fungu la Serikali kupitia TARURA au TANROADS.

"Na barabara ile ilikwishatengenezwa wakati huo yeye (Dkt.Slaa) akiwa Balozi huko Sweden, hakuwahi kutoka na kulalamikia kitendo hicho alikifanya Hayati Dkt.Magufuli cha kutengeneza na kuahidi hadharani ujenzi wa barabara hiyo.

"Huku sadaka akitoa madhabauni hapo kanisani na akiwa si mshirika wa kanisa hilo, Dkt.Slaa alikuwa kimya.

"Ninashangaa kwa nini Dkt.Slaa alikuwa kimya, Magufuli alikesha kutengeneza makanisa mbalimbali, kutoa sadaka makanisani hususani Katoliki.

"Magufuli alishawishi kuchanga fedha kwa ajili ya kujengwa msikiti kule Dodoma, alishawishi ujenzi wa BAKWATA pale Kinondoni jijini Dar es Salaa.

"Hayati Dkt.Magufuli alishawishi mambo mengi hayo, lakini Dkt.Slaa hakuwahi kusema, lakini ameendelea kumshangaa Mama Samia na kutaja kwamba amechanga milioni 100 na milioni 150.

"Inaonekana kuna chuki binafsi kati yake dhidi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan.

"Hivyo basi kutokana na kauli hiyo, ninakubaliana kabisa kwamba Dkt.Slaa ameendelea kutafuta namna gani ya kumchafua Mheshimiwa Rais Dkt.Samia na sababu za kuchafuliwa huko bado hatuzijui na kwa nini ameanza kumchafua kwa muda mrefu.

"Ni kabla hata hajavuliwa hadhi ya Ubalozi, hivyo nimuombe Dkt.Slaa kuanzia sasa amuache Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan afanye kazi zake.

"Amsubiri akimaliza kazi zake na kustaafu ndipo aanze kusema mambo ambayo hakuyapenda ambayo anayafanya au atumie haki yake ya Kikatiba katika Uchaguzi endapo Mama Samia atagombea ili amyime kura au asipige kura dhidi yake.

"Ndiyo nafasi aliyonayo ya Kikatiba na sio kuingilia shughuli zake, amuache Mheshimiwa Rais Dkt.Samia aendelee kusaidia wananchi wake na makundi mbalimbali katika jamii kadri anavyoweza,"amefafanua Mwinjilisti Temba.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news