DAR ES SALAAM-Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Emmanuel Tutuba, amekutana na Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Mhe. Christine Grau katika ofisi za Benki Kuu jijini Dar es Salaam.
Viongozi hao kwa pamoja wamejadiliana masuala mbalimbali kuhusu uchumi wetu ikiwemo kuanza kwa mfumo wa utekelezaji wa sera ya fedha unaotumia riba, ukuaji wa huduma jumuishi za fedha pamoja na uboreshwaji wa mifumo ya malipo.
Katika kikao hicho, Gavana Tutuba ameuomba umoja huo kuwajengea uwezo zaidi wafanyakazi wa Benki Kuu na kubadilishana uzoefu katika masuala mbalimbali ya fedha na uchumi ili waweze kutimiza majukumu yao kwa ufanisi zaidi.