DAR ES SALAAM-Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Emmanuel Tutuba, amekutana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Watumishi Housing Investiment (WHI), Dkt. Fred Msemwa.
Ni katika ofisi za Benki Kuu jijini Dar es Salaam na kujadiliana masuala mbalimbali kuhusu uendeshaji wa taasisi hiyo iliyoanzishwa mwaka 2014 kwa ajili ya kutekeleza mpango wa makazi kwa watumishi wa umma na wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii.
Aidha, Gavana Tutuba alipata fursa ya kufahamu namna WHI inasimamia Mifuko ya Uwekezaji ambayo ni Mfuko wa Uwekezaji katika Milki (REIT) na Mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja (CIS) ambapo kwa sasa WHI inaendesha MFUKO WA FAIDA.
Pamoja na mambo mengine, Gavana ametoa wito kwa taasisi hiyo kubuni mikopo mbalmbali ili kukidhi mahitaji ya wateja pamoja na kushirikiana na sekta ya fedha ili kuwezesha upatikanaji wa nyumba bora kwa watumishi wa umma.