Huyu hapa Katibu Mkuu mpya wa CCM, Balozi Dkt.Emmanuel John Nchimbi

ZANZIBAR-Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa kimepokea pendekezo la Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa kuhusu jina la Katibu Mkuu wa CCM.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu. Samia Suluhu Hassan, akizungumza jambo na Katibu Mkuu mpya wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Emmanuel John Nchimbi mara baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo kwenye Kikao Maalum cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kilichokutana tarehe 15 Januari, 2024 Mjini Unguja Zanzibar.Bofya hapa, mfahamu Balozi Dkt.Emmanuel John Nchimbi

"Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa imefanya kikao Maalum tarehe 15 Januari, 2024, Zanzibar, chini ya Mwenyekiti wake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Kikao hicho kilitanguliwa na Semina kwa Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa kuanzia tarehe 13 – 14 Januari, 2024. Katika Semina hiyo wajumbe walipewa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya kimkakati na kuridhishwa na maendeleo ya utekelezaji wake ikiwemo: –

1. Mradi wa Bwawa la Umeme wa Julius Nyerere (JHPP) na mipango ya kuboresha hali ya umeme Nchini.


2. Mradi wa Reli ya “Standard Gauge Railway (SGR)”.

3. Ujenzi wa daraja la John Pombe Magufuli (Kigongo – Busisi).

4. Utekelezaji wa Ilani ya CCM, kwa upande wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ).

5. Hali ya Mashirika ya Umma Nchini na Mageuzi yanayohitajika.

Pamoja na mambo mengine, kikao hicho kilipokea taarifa mbalimbali ikiwemo: –

1. Maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji mwaka 2024.

2. Maandalizi ya Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 47 ya Kuzaliwa kwa CCM;

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Januari 15,2024 na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa,Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Paul Makonda.


Amesema,wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa wameridhia kwa kauli moja pendekezo hilo na kumchagua ndugu Balozi mstaafu Dkt. Emmanuel John Nchimbi kuwa Katibu Mkuu wa CCM.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu. Samia Suluhu Hassan, akizungumza kwenye Kikao Maalum cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kilichokutana tarehe 15 Januari, 2024 Mjini Unguja Zanzibar. Kulia ni Katibu Mkuu mpya wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Emmanuel John Nchimbi.
Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa kimeipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Ndugu Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa kuendelea kutekeleza kwa ufanisi Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025 kwa upande wa Zanzibar na kufanikisha Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.


Vile vile, kikao hicho kimepongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan kuendelea kutekeleza kwa ufanisi Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020 – 2025.
Katibu Mkuu mpya wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Emmanuel John Nchimbi akizungumza kwa mara ya kwanza mara baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo kwenye Kikao Maalum cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kilichokutana tarehe 15 Januari, 2024 Mjini Unguja Zanzibar.
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza katika kikao hicho kulichofanyika Zanzibar Leo Jumatatu 15.2024.
Katibu Mkuu mpya wa Chama cha Mapinduzi CCM ndugu Emmanuel John Nchimbi akiwa na sura ya bashasha mara baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo kwenye Kikao Maalum cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kilichokutana tarehe 15 Januari, 2024 mjini Unguja Zanzibar.
Wajumbe mbalimbali wakati wa Kikao Maalum cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kilichokutana tarehe 15 Januari, 2024 Mjini Unguja Zanzibar. Bofya hapa, mfahamu Balozi Dkt.Emmanuel John Nchimbi

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news