DAR ES SALAAM-Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa, Mhe. Stanlaus Mabula amezitaka halmashauri kusimamia kikamilifu miradi inayotekelezwa na wataalamu wa ndani(force akaunt) ili ilite tija kwa wananchi.
Mhe. Mabula ameyasema hayo Januari 27, 2024 wakati wa ziara ya Kamati ya LAAC kwenye Halmashauri za Ubungo na Kinondoni kukagua utekelezaji wa miradi ya afya msingi.
Amesema, kamati imetembelea hospitali za Manispaa ya Ubungo na Kinondoni ambazo moja imejengwa kwa kutumia Force Account na nyingine baadhi ya majengo yamejengwa na mkandarasi.
"Tumelinganisha gharama na ubora tunachosisiza muongeze usimamizi. Miradi yote imetekelezwa kwa ubora changamoto ni ndogo ndogo tu ambazo mnatakiwa kwenda kurekebisha na mzizingatie katika miradi mingine ili isije ikajitokeza na piatija iliyotegemewa iweze kupatikana."
"Rais Samia ametoa fedha nyingi kwenye miradi ya afya na elimu ambayo mingi inatekelezwa kwenye halmashauri zenu sasa inatakiwa watu waone kwa vitendo matumizi ya fedha hizo kupitia miradi ambayo itasaidia kutoa huduma bora kwa wananchi."
Naye Naibu Waziri, Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Mhe. Dkt. Festo Dugange ameishukuru Kamati kwa kutembelea miradi ya afya na kuahidi kufanyia kazi maelekezo yote yaliyotewa.
Kamati wa LAAC wakiwa mkoani Dar es salaam wametembelea hospitali ya Manispaa ya Ubungo, Kituo cha Afya Makuburi, Kituo cha Afya Kinondoni na Hospitali ya Manispaa ya Kinondoni iliyopo Mabwepande.