🔴LIVE:NECTA ikitangaza Matokeo ya Upimaji wa Kitaifa wa Kidato cha Pili na Darasa la Nne 2023

NA GODFREY NNKO

BARAZA la Mitihani la Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya Upimaji wa Kitaifa wa Kidato cha Pili (FTNA) pamoja na matokeo ya Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Nne (SFNA).
Matokeo hayo yametangazwa leo Jumapili Desemba 7, 2023 jijini Dar es Salaam na Katibu Mtendaji wa NECTA,Dkt.Said Ally Mohamed.

Amesema, katika mkutano wake wa 157 uliofanyika Januari 7,2024 katika Ofisi za Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) zilizopo jijini Dar es Salaam, baraza hilo limeidhinishwa kutangazwa rasmi kwa matokeo hayo.

Amesema, upimaji huo ulifanyika mwezi Oktoba na Novemba 2023 ambapo kuhusu usajili na mahudhurio jumla ya 1,693,444 walisajiliwa kufanya upimaji wa Darasa la Nne wakiwemo wasichana 864,482 sawa na asilimia 51.

Huku wavulana wakiwa ni 828,962 sawa na asilimia 49 ya wanafunzui hao ambao walipima kupitia mtihani huo wa darasa la nne.

Dkt.Mohamed amesema, mahudhurio katika upimaji huo wa darasa la nne yalikuwa asilimia 92.3 sawa na wanafunzi 1,545,607.

Aidha, wanafunzi 147,837 sawa na asilimia 8.7 hawakufanya upimaji huo licha ya kusajiliwa kufanya mitihani hiyo ya upimaji.

Amesema, jumla ya wanafunzi 1,287,934 kati ya 1,545,330 wenye matokeo sawa na asilimia 83.34 wamefaulu kwa kupata madaraja ya A, B, C na D. 

“Mwaka 2022 wanafunzi waliofaulu walikuwa 1,320,700 sawa na asilimia 82.95, hivyo, kumekuwa na ongezeko la ufaulu kwa asilimia 0.39 kwa wanafunzi waliopata fursa ya kuendelea na darasa la tano ikilinganishwa na mwaka 2022.

“Kati ya wanafunzi waliofaulu kuendelea na darasa la tano,wasichana ni 681.259 sawa na asilimia 8.79  na wavulana ni 606,675 sawa na asilimia 8.78, takwimu zinaonesha kuwa, wasichana wamefaulu vizuri ikilinganishwa na wavulana,"amesema Dkt.Mohamed.

Kwa upande wa matokeo ya upimaji wa kitaifa wa kidato cha pili, jumla ya wanafunzi 592,741 kati ya 694,769 wenye matokeo ambao ni sawa na asilimia 85.31 wamefaulu ambapo wamepata madaraja ya I, II, III na IV.

“Mwaka 2022 wanafunzi waliofaulu walikuwa 539,645 sawa na asilimia 85.1, hivyo kumekuwa na ongezeko la ufaulu kwa asilimia 0.13 pamoja na ongezeko la idadi ya wanafunzi 53,096 sawa na asilimia 9.84 ya wanafunzi waliopata fursa ya kuendelea na kidato cha tatu ikilinganishwa na mwaka 2022.

“Kati ya wanafunzi waliofaulu kuendelea na kidato cha tatu, wasichana ni 314,949 sawa na asilimia 83.66 na wavulana ni 277,792 sawa na asilimia 87.28, takwimu zinaonesha kuwa, wavulana wamefaulu vizuri ikilinganishwa na wasichana,"amesema Katibu Mtendaji huyo.

Wakati huo huo, NECTA imefuta matokeo ya wanafunzi 178 wa darasa la nne na 28 wa kidato cha pili kwa kufanya udanganyifu kwenye karatasi zao za upimaji kitaifa katika mitihani hiyo.

“Matokeo hayo yamefutwa kwa mujibu wa Kifungu cha 5 (2) () cha Sheria ya Baraza la Mitihani sura ya 107 kikisomwa pamoja na Kifungu cha 30(2) (b) 2016 cha Kanuni za Mitihani,”amesema Katibu Mtendaji huyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news