DAR ES SALAAM-Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI),Mheshimiwa Mohamed Mchengerwa amekutana na uongozi wa TARURA na wataalamu wengine kwa ajili ya kujadiliana kuhusu changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika miundombinu ya barabara nchini.
Ameyasema hayo leo Januari 23, 2023 katika kikao chake na menejimenti ya Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), wataalam washauri na wakandarasi.Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Juliusu Nyerere jijini Dar es Salaam (JNICC).
“Hii ni mara yangu ya kwanza kukutana nanyi katika umoja huu, tangu niteuliwe kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI,japo ninaamini baadhi yenu tumekutano sehemu mbalimbali katika shughuli za ujenzi wa Taifa.
“Tunakutana hapa ili kujadili changamoto zinazojitokeza katika ujenzi, ukarabati na matengenezo ya miundombinu ya barabara za wilaya nchini zilizo chini ya TARURA;