Maafa ya mvua Dar, Serikali yaingia kazini

DAR ES SALAAM-Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulika na Sera, Bunge na Uratibu, Mhe. Ummy Nderiananga amepongeza Kamati ya Maafa ya Mkoa wa Dar es Salaam kwa jitihada mbalimbali za kurejesha hali katika maeneo ambayo miundombinu ya barabara imeathirika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulika na Sera, Bunge na Uratibu Uratibu, Mhe. Ummy Nderianga alipotembelea kuona maungio ya daraja la Kunduchi barabara ya Kunduchi yalioathirika kutokana na mvua za vuli zinazoendelea kunyesha katika Jiji la Dar es Saalam.

Kauli hiyo ameitoa wakati wa ziara yake leo Januri 21,2024 mkoani humo alipotemebelea na kujionea athari za mvua zilizonyesha usiku wa kuamkia Januari 20,2024 na kuathiri maeneo mabalimbali ya wilaya ya Kindondoni, Temeke, Kigamboni, Ubungo na Jiji la Ilala.

Naibu Waziri Ummy amesema, anampongeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mhe. Abert Chalamila kwa uongozi ambao wameuonesha katika kurejesha halina kazi waliyofanya.

“Naomba tufanye kazi hii usiku na mchana ili tuweze kurejesha hali mapema bila kuathiri shughuli za biashara na shughuli nyingine za uchumi zinazofanyika katika Mkoa wa Dar es saalam,” amehimiza.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulika na Sera, Bunge na Uratibu Uratibu Mhe. Ummy Nderianga akielekeza jambo kwa mratibu wa maafa mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Gerad Sondo wakati alipotembelea kujionea juhudi za urejeshaji hali katika maungio ya Daraja la Mbopo barabara ya Madale katika jiji la Dar es salaam.
Katika picha ni baadhi ya maungio ya madaraja ambayo yameathrirka kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha na juhudi kubwa zikifanywa na serikali usiku na mchana katika kurejesha mawasiliano ya barabara katika maeneo ya maungio ya madaraja hayo ili yaendelee kupitika.

"Sisi kama serikali tunawahakikishia wana Dar es salamu kwamba tutafanya kazi hii ya urejeshaji wa hali kwa nguvu bila kuchoka,"amesema.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kindondoni, Mhe. Saad Mtambule amesema, kazi waliyofanya ni kusimamia usafishaji wa mitaro na usawishaji wa mito na hivyo kusaidia maji kutotuwama kwa muda mrefu.

“Tumeendelea kuwaeleza wananchi walio katika maeneo ya pembezoni mwa mito kama; Mto Nyakasangwa, Mto Mpiji, Mto Tegeta, Mto Mlalakuwa na Mto Ng’ombe kuhamia maeneo ya juu ili kuepeuka athari za mvua,”amebainisha.

Ujenzi wa nyumba holela umesababisha watu kujenga mpaka kwenye mapito asili ya maji na kusababisha maji kukosa sehemu za kupita na kuingia maeneo ya watu.
Katika picha ni baadhi ya maungio ya madaraja ambayo yameathrirka kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha na juhudi kubwa zikifanywa na serikali usiku na mchana katika kurejesha mawasiliano ya barabara katika maeneo ya maungio ya madaraja hayo ili yaendelee kupitika.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulika na Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderianga akiwa amembeba mtoto wakati alipotembelea kuona urejeshaji wa maungio ya daraja katika ya barabara ya Tanganyika katika daraja la Mbweni yaliyoathiriwa kutokana na Mvua za vuli zinazoendelea kunyesha jijini Dar es salaam.

“Lakini pia tuna kazi ya kuendelea kuwaelimisha wananchi ili wafuate misingi ya ujenzi wa maeneo kulingana na ramani ya mipango miji,” amesisitiza

Akizungumza katika ziara hiyo Mkazi wa Ununio, Bw. James Koyi ameishukuru serikali kwa kazi kubwa inayofanya ya urejeshajji wa hali katika maeneo yaliyoathirika mafuriko kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha mkoa wa Dar es salaam.
"Hakuna aliyejua kama mvua itanyesha masaa ishirini na nne hata hivyo serikali iendelee kufanya kazi katika kurejesha hali,"amesema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news